Posts

Showing posts from April, 2023

21 - Baba Twakujia

21 - Baba Twakujia "Father, We Come To Thee" 1. Baba twakujia, Uwe msaada; Uwe kimbilio, twakusihi. Dunia ni giza tukitengwa nawe; Fufariji hapa, Baba yetu. Baba twakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie. 2. Salama tulinde, kati ya taabu; Uwe raha yetu mashakani. Roho ya sumbuka, Baba tujalie; Twakuomba sana, tupe nguvu. 3. Neema utupe, tukubali kwako; Moyo wetu Linda, safarini; Tuongoe mbele, tupate kushinda Na kufika ng`ambo, kule kwako.  ( Amina)

22 - Usinipite Mwokozi

22 - Usinipite Mwokozi "Pass Me Not" 1. Usinipite , Mwokozi, unisikie; Unapozuru wengine, usinipite. Bwana, Bwana, unisikie; Unapozuru wengine, usinipite. 2. Kiti chako cha rehema, nakitazama; Magoti napiga pale, nisamehewe. 3. Sina ya kutegemea, ila wewe tu; Uso wako uwe kwangu, nakuabudu. 4. Wewe tu u mfariji: sina mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine.   ( Amina)

23 - Yesu Furaha Ya Moyo

23 - Yesu Furaha Ya Moyo "Jesus ,Thou Joy Of Loving Hearts" 1. Yesu, furaha ya moyo!Hazina ya pendo, na nuru. Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe. 2. Kweli yako ya daima, wawajibu wakuitao, Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao. 3. U Mkate wa uzima, kupokea ni baraka, Twanywa kwako u kisima roho zikiburudika. 4. Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia; Twakushika kwa imani, nawe watubariki. 5. Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima; Giza ya dhambi fukuza uwe mwanga wa uzima.   ( Amina)

24 - Jina Lake Yesu Tamu

24 - Jina Lake Yesu Tamu "How Sweet The Name Of Jesus" 1. Jina lake Yesu tamu Tukilisikia, Hutupoza, tena hamu Hutuondolea, 2. Roho iliyo umia kwalom hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka. 3. Jina hili nimsingi, Ngao, Ngoma, Mwamba, Kwa hili napata ungi, kwangu ni akiba. 4. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, na Amana, Mali yangu yote! 5. Moyo wangu hauwezi kukusifu kweli; Ila sifa zangu hizi, Bwana, zikubali.    (Amina)

25 - Taji Mvikeni

25 - Taji Mvikeni "Crown Him With Many Crowns" 1. Taji mvikeni Taji nyingisana, kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana; Nami tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu. 2. Taji mvikeni Mwanawa bikira; Anazovaa kicwani Aliteka nyara; Shilo wa manabii Mchunga wa watu Shina na tanzu vya Yese Wa Bethilehemu. 3. Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake nishani Ni vito vya enzi, Mbingu haina Hta malaika Awezaye kuziona pasipo kushangaa! 4. Taji mvikeni Bwana wa Salama; Kote-kote duniani Vita vitakoma; Nayo enzi yake Itaendelea, Chini ya miguu yake, Maua humea.   (Amina)

26 - Tupe Amani

26 - Tupe Amani "God The Omnipotent" 1. Mungu mtukufu Aliyeumba Pepo kuvuma Na radi kali; Toa neema unapotawala, Tupe amni, Bwana wa wema. 2. Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno Lako; Hasira zoko Zitaharibu, , Tupe amni, Bwana wa wema. 3. Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu Wako; Lakini wema wako utadumu; Endesha wema Bwana wa wema. 4. Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako; Hivi tunaziimba sifa zako; Wako uwezo na utukufu.  (Amina)

27 - Tena, Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako

27 - Tena, Mwokozi, Twalitukuza Jina Lako "Saviour Again To Thy Dear Name" 1. Tena, Mwokozi, twalitukuza jina lako lenye kupendeza, Twangojea neno la amani, Kabla hatujakwenda nyumbani. 2. Tupe amani njiani mwetu, Wewe umwanzo, umwisho wetu; Dhambini kamwe isiingie Midomo ikutaye wewe. 3. Utupe amani usiku huu, Ili gizani kuwe nuru kuu. Tulinde kwa kuwa kwako Bwana. Usiku nisawa na mchana. 4. Tupe amani ulimwenguni Ndiyo dawa yetu majonzini; Na ikitwita sauti yako, Tupe amani milele kwako.  (Amina)

28 - Jina La Thamani

28 - Jina La Thamani "Take The Name Of Jesus' 1. Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni; Litakufariji ndugu,Enda nalo popote. Jina la Thamani, (Thamani)  (thamani) Tumai la dunia Jina la thamani - - tamu!) Furaha ya mbinguni. 2. Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani. Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili. 3. Jina hili la thamani Linatufurahisha,  Napotukaribisha, Na tunapomwimbia. 4. Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu. Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.   (Amina)

29 - Yesu, Nakupenda

29 - Yesu, Nakupenda "My Jesus I Love" 1. Yesu nakupenda, u mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu: Na mwokozi aliyeniokoa Sasa nakupenda, kuzidi pia. 2. Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia. 3. Ulipoangikwa msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia. 4. Mawanda mazuri na masikani Niyatzamapo huko mbinguni, `Tasema na taji nitakayovaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   (Amina)

30 - Yesu Unipendaye

30 - Yesu Unipendaye "Jesus, Lover Of My Soul" 1. Yesu unipendaye kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye mwovu akinijia. Yafiche ubavuni mwako maisha yangu; Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu. 2. Ngome nyingine sina; nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako, Ninakuamania, kuniweshesha; Shari wanikingia, vitani wanitosha. 3. Nakutaka mpaji, vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, utanijazi vyako; Nao waangukao wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, uongoze vipofu. 4. Bwana umeniosha moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha yapatikana kwako; Kwako Bwana naona kisima cha uzima; Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.   (Amina)

31 - Niimbe Pendo Lake

 31 - Niimbe Pendo Lake "I will Sing Of Jesus" 1. Niimbe (niimbe) pendo lake, Pendo la (pendo la) Yesu Bwana; Sababu (sababu) alitoka Kwa Baba, akafa. Niimbe (niimbe) pendo lake; Sifa kuu (sifa kuu) nitatoa; Akafa (akafa) niwe hai, - - Niimbe pendo lake. 2. Machozi 9machozi) alitoa Ijapo (ijapo) sijalia; Maombi (maombi) yangu bado, Aniombeapo. 3. Upendo (upendo) kubwa huo! Dunia (dunia) haijui Samaha (samaha) kwa makosa Kubwa kama yangu. 4. Hapana (hapana) tendo jema Ambalo (ambalo) nilitenda, Nataka (nataka) toka leo Nimwonyeshe pendo. (Amina)

032 - Tangu Kuamini

  032 - Tangu Kuamini "I Have A Song I Love To Sing" 1. Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini; Wa mkombozi, Mfalme, Tangu kuamini. Tangu kuamini, Jina lake `tasifu, Tangu kuamini, Nitalisifu Jina lake. 2. Kristo anitosha kweli, Tangu kuamini, Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini. 3. Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini, Linalofukuza shaka, Tangu kuamini. 4. Ninalo kao tayari, Tangu kuamini, Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini. (Amina)

33 - Karibu Sana

33 - Karibu Sana "Neare, Still Nearer" 1. Karibu sana univute, karibu sana daima niwe. Bwana napenda unishike, Unilinde nisitengwe nawe, Unilinde nisitengwe nawe. 2. Karibu sana, sina kitu, Sina sadaka kwa Bwana Yesu, Isipokuwa moyo wangu: Uutakase katika damu, Uutakase katika damu. 3. Karibu sana wewe, wewe nami, Nitafurahi kuacha Dhambi- - Anasa zote na kiburi: Nipe Yesu niliye msulibi, Nipe Yesu niliye msulibi. 4. Karibu sana, hata mwisho. Hata mbinguni nisimamapo: Daima dawamu niwepo Nitakapoona uso wako,      Nitakapoona uso wako.   (Amina)

34 - Hadithi Kisa Yesu

  34 - Hadithi Kisa Yesu "Tell Me The Story Of Jesus" 1. Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana; Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa. Jinsi malaika wengi walivyoimba sifa, Alipoleta amani kwa watu wa dunia. Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu; Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa. 2. Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani. Jinsi alivyolishinda jaribu la shetani; Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni, Jinsi walivyomtesa: Yote ni yaajabu! 3. Habari za msalaba Aliposulubishwa: Jinsi walivyomzika Akashinda kaburi. Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu, Aliye toa maisha Nipokee wokovu. (Amina)

35 - Nimekombolewa Na Yesu

 35 - Nimekombolewa Na Yesu "Redeemed! How I Love To Proclaim It" 1. Nimekombolewa na Yesu na sasa nimefurahi; Kwa bei ya mauti yake mimi ni mtoto wake. Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! mimi mwana wake kweli. 2. Kukombolewa nafurahi, kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake. 3. Nitamwona Mfalme wangu, katika uzuri wake; Ambaye najifurahisha katika torati yake. 4. Najua taji imewekwa mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, ili alipo, niwepo. (Amina)

36 - Siku Kuu

36 - Siku Kuu "O Happy Day" 1. Ni siku kuu siku ile ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, kunyamaza hauwezi. Siku kuu! Siku kuu ya kuoshwa dhambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, aniongoza miguu. Siku kuu! siku kuu ya kuoshwa dhambi zangu kuu! 2. Tumekwisha patina, mimi mbwake, yeye mbwangu, Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu. 3. Moyo tulia kwa Bwana, kiini cha raha yako: Huna njia mbili tena: uwe naye, yote ndako.   (Amina)

37 - Pendo Lako, Ee Mwokozi

37 - Pendo Lako, Ee Mwokozi "Love Divine, All Loves Excelling" 1. Pendo lako , Ee Mwokozi, Hushinda pendo zote! Kaa nasi, ndani yetu, Furaha ya mbinguni. Yesu, u rehema tupu, Safi, na kusamehe, Mfariji mwenye huzuni Ziondoe machozi. 2. Roho yako ya upendo Tuma kwa kundi lako; Hebu tuirithi raha, Iliyoahidiwa. Uondoe moyo mbaya, U Mwanzo, tena Mwisho; Timiza imani yetu, Ilituwekwe `huru. 3. Yesu, uje kwetu sasa, Tupokee huruma; Rudi kwetu, tena kamwe Usituache pekee. Tungekutukuza leo, pamoja na malaika, Imba na kutoa sifa, Ingia kwa ibada. 4. Sasa, Bwana, kazi yako, Imalize moyoni; Takasa hekalu lako, Wokovu kamilisha! Safisha viumbe vyako Katika wakati huu; Tupumzike `toka dhambi, Tuingie mbinguni. (Amina)

38 - Nasifu Shani Ya Mungu

  38 - Nasifu Shani Ya Mungu "I Sing The Mighthy Power" 1. Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari, Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi, Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho. 2. Kadri ya nionayo, ya kusifu Mungu; Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu; Hakuna hata unyasi, usiokuza; Na upepo wavumisha,  au kutuliza. 3. Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa, Ni pato nikusifupokukwomba ni dawa; Umenizingira nyuma, na mbele baraka; Maarifa ya ajabu! Yanishinda mimi!   (Amina)

39 - Ati, Kuna Mvua Njema

39 - Ati, Kuna Mvua Njema "Lord, I Hear Of Showers" 1. Ati, kuna mvua njema yenye neema; Watu wanaona vyema Bwana, huninyeshei? Na mimi? Na mimi? Bwana, huninyeshei? 2. Sinipite, Baba mwema; dhambini nimezama: Rehema ni za daima; Bwana hunionyeshi? 3. Sinipite, Yesu mwema; niwe nawe daima, Natamani kukwandama: Bwana, hunichukui? 4. Sinipite, Roho mwema, Mpaji wa uzima, Nawe shahidi wa wema, Bwana wema hunipi?   (Amina)

40 - Nijaze Sasa

40 - Nijaze Sasa "Hover O'er Me Holy Spirit" 1. Njoo, Roho Mtukufu uoshe moyo wangu, Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa. Roho Mtukufu, njoo, nijaze sasa. Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa. 2. Ujalize moyo wangu Ijapo sikuoni, Nami ninakuhitaji, njoo, nijaze sasa. 3. Nimejaa udhaifu, ninainamia kwako; Roho Mtukufu sasa, nitilie na nguvu. 4. Unioshe, nifariji, niponye nibariki, Unijaze moyo wangu: ndiwe mwenye uwezo. (Amina)

41 - Roho Mtakatifu

41 - Roho Mtakatifu "Holy Spirit Faithful Guide" 1. Roho Mtakatifu, Kiongozi amini; Utushike mkono Tulio wasafiri; Utupe kusikia Sauti ya upole; "Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani." 2. Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu; Tusiache shakani; Tukiwa gizani Utupe kusikia Sauti ya upole; "Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani." 3. Siku zetu za kazi, Zikiwa zimekwisha, Wala hatuna tama Ila mbingu na sala: Utupe kusikia Sauti ya upole; "Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."   (Amina)

42 - Ewe Roho Wa Mbinguni

42 - Ewe Roho Wa Mbinguni "Spirit Divine, Attend Our Prayer" 1. Ewe Roho wa Mbinguni, Maombi sikia! Makao yako yafanye Mioyoni mwetu. 2. Kama nuru, tupenyeze, Giza uondoe; Siri yako tuione, Na amani yako. 3. Kama moto, tusafishe, Choma dhambi yetu; Roho zetu zote ziwe Hekalu la Bwana. 4. Kama umande, na uje, Utuburudishe, Moyo `kavu utakuwa Ni wenye  baraka. 5. Kama upepo Ee Roho, Katika Pente koste Ukombozi utangaze, Kwa kila taifa.   (Amina)

43 - Furaha Gani!

43 - Furaha Gani! "What A Fellowship!" 1. Furaha gain na ushiriki, Nikimtegemea Yesu tu! Baraka gain, tena amani, Nikimtegemea Yesu tu! Tegemea, salama bila hatari; Tegemea, tegemea  Mwokozi Yesu. 2. Nitaiweza njia nyembamba, Nikimtegemea Yesu tu; Njia `tazidi kuwa rahisi, Nikimtegemea Yesu tu. 3. Sina sababu ya kuogopa, Nikimtegemea Yesu tu; Atakuwa karibu daima, Nikimtegemea Yesu tu.   (Amina)

44 - Urafiki Wa Yesu

44 - Urafiki Wa Yesu 'There's Not A Friend" 1. Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna! Tabibu mwingine wa rohoni, Hakuna, hakuna! Yesu ajua shida zetu; Daima ataongoza Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna! 2. Wakati ambapo hapo yeye, Hapana, hapana! Wala giza kututenga naye, Hapana, hapana! 3. Aliye sahauliwa naye, Hakuna, hakuna! Mkosaji asiyempenda, Hakuna, hakuna! 4. Kipawa kama Mwokozi wetu, Hakuna, hakuna! Ambaye atanyimwa wokovu, Hakuna, hakuna!   (Amina)

45 - Mwanga Umo Moyoni

45 - Mwanga Umo Moyoni "Sunlight In The Heart" 1. Mlimani pana mwanga, Mwanga wa jua zuri Shambani na baharini Jua tukufu liko; Mwanga uliyo mkubwa Umo moyoni mwangu, Kwa kuwa Yesu alipo Hapa pana mwangaza. Mwangaza ulio mzuri. Mwanga umo moyoni; Akiwapo Bwana Yesu Pana mwanga moyoni. 2. Kama mavazi kikuu, Ninavua huzuni: Nguo nzuri za kuvaa, Umenipa za kuvaa. Nakuandama rohoni Hatanyumba ya juu Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako. 3. Ulinikomboa Yesu; Maisha yangu, mali, Vyote nivyako, Mwokozi Daima nikusifu. Nakuandama rohoni Hatanyumba ya juu Iliyopambwa vizuri Katika pendo lako.   (Amina)