41 - Roho Mtakatifu

41 - Roho Mtakatifu
"Holy Spirit Faithful Guide"

1.

Roho Mtakatifu, Kiongozi amini;
Utushike mkono Tulio wasafiri;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."

2.

Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu;
Tusiache shakani; Tukiwa gizani
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."

3.

Siku zetu za kazi, Zikiwa zimekwisha,
Wala hatuna tama Ila mbingu na sala:
Utupe kusikia Sauti ya upole;
"Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani."

 (Amina)

Comments

Popular posts from this blog

24 - Jina Lake Yesu Tamu

26 - Tupe Amani

22 - Usinipite Mwokozi